Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, taarifa iliyotolewa na uongozi wa taasisi hiyo, inaelezea kwamba; Hawza hiyo inatoa masomo ya Hawza yaani elimu ya dini ya Kiislamu, pamoja na mafunzo ya kompyuta na skauti, yote yakilenga kuwajengea vijana maarifa ya kidini, ujuzi wa kisasa na nidhamu ya maisha. Mafunzo hayo yanatolewa kwa vijana wa kiume.
Uongozi wa Hawza umeeleza kuwa lengo kuu la programu hizo ni kuandaa kizazi chenye misingi imara ya dini, chenye uwezo wa kutumia teknolojia ya kisasa, pamoja na kuwaandaa vijana kuwa viongozi bora wa baadaye katika jamii.
Wananchi wote, wazazi na walezi wa vijana wanaokidhi vigezo wanahimizwa kujitokeza kwa wingi ili kuwanufaisha vijana wao kupitia fursa hii muhimu ya kielimu na kimaadili.
Mwisho wa usajili
Uongozi wa Hawza umetangaza kuwa mwisho wa usajili ni tarehe 1 Januari 2026, na kuwataka wote wanaokusudia kujiunga kuzingatia muda uliopangwa ili kuepuka usumbufu.

Maoni yako